NIGER-USALAMA

Niger: Raia 14 wauawa katika shambulio karibu na mpaka wa Mali

Wanajesi wa Niger wakipiga doria.
Wanajesi wa Niger wakipiga doria. ISSOUF SANOGO / AFP

Watu 14 waliuawa Jumapili nchini Niger katika shambulio huko Banibangou magharibi mwa nchi hiyo, karibu na mpaka na Mali, mamlaka imesema leo Jumanne katika taarifa.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lilitolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani katika taarifa iliyosomwa kwenye redio ya umma. Kulingana na wizara hiyo, shambulio hilo lilitekelezwa Jumapili mwendo wa saa tatu usiku na "watu wasiojulikana, wakiwa na silaha na ambao walikuwa kwenye pikipiki".

Wizara ya Mambo ya Ndani imetaja shambulio hilo kama "la kinyama" na imetangaza "hatua za ukisalama na kiafya zilizoimarishwa katika eneo hilo" na vile vile "kufunguliwa kwa uchunguzi.