SUDANI KUSINI

Umoja wa Mataifa waitaka Sudan kokomesha mauaji dhidi ya raia

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akilihutubia taifa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 10 ya uhuru wa Sudan Kusini, State House, huko Juba, Julai 9, 2021.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akilihutubia taifa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 10 ya uhuru wa Sudan Kusini, State House, huko Juba, Julai 9, 2021. REUTERS - JOK SOLOMUN

Umoja wa Mataifa unataka kusitishwa kwa mauaji ya kiholela nchini Sudan Kusini baada ya kuuliwa kwa watu 42, wakiwemo wavulana katika taifa hilo changa duniani.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, umebaini kuwa, miongoni mwa watu, waliuliwa mbele ya familia za,o huku wengine wakifungwa mtini na kupigwa risasi.

Tangu mwezi Machi mwaka huu, wachunguzi wamebaini kuwa watu 29 waliokuwa wameshukiwa kuhusika na makosa mbalimbali, waliouwa katika jimbo la Warrap, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Watu hao wakiwemo wazee na wavulana, waliondolewa gerezani au vituo vya Polisi na kuuawa hata bila kufikishwa Mahakamani.

Mauaji ya watu wengine 13 yalitokea katikati ya mwezi Juni katika Jimbo la Lakes.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom, amelaani mauaji hayo na kutaka uchunguzi kufanyika na waliohusika na mauaji hayo kufunguliwa kuchukuliwa hatua za kisheria.