DRC-SIASA

Viongozi wa dini watofautiana kuhusu jina la atakayeongoza CENI DRC

Denis Kadima, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Uchaguzi kuhusu Demokrasia Endelevu barani Afrika, na mgombea kwenye kiti cha mkuu wa CENI kutoka Kanisa la Kimbanguist, huko Kinshasa, Julai 28, 2021.
Denis Kadima, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Uchaguzi kuhusu Demokrasia Endelevu barani Afrika, na mgombea kwenye kiti cha mkuu wa CENI kutoka Kanisa la Kimbanguist, huko Kinshasa, Julai 28, 2021. © Sonia Rolley/RFI

Viongozi wa dini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameshindwa kuja na jina moja la Mwenyeketi mpya wa Tume ya Uchaguzi nchini humo CENI, baada ya mazungumzo ya siku kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, viongozi wanane wa dini kutoka madhehebu ya Kikiristo na dini ya Kiislamu walikutana kwenye makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, lakini wakashindwa kuafikiana kuhusu ni nani aongoze Tume hiyo.

Mvutano ulianza pale, viongozi wa Kanisa Katolilki na Kiprotestanti walipoomba muda zaidi wa kupitiwa kwa majina ya baadhi ya wagombea, kinyume na mtazamo wa  vongozi wa madhehebu mengine sita.

Hata hivyo, viongozi hao wa dini hawakueleza kwa kina kuhusu tofauti zao huku wakisisitiza kuwa, wako pamoja na watawasilisha ripoti ya mwisho bungeni siku ya Jumatano.

Mpaka sasa, hakuna jina rasmi lililotajwa lakini duru zinasema kuwa viongozi wengi wamependekeza jina la Denis Kadima, ambaye viongozi wa Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiprotestanti wanaomwona mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi.