TUNISiA-SIASA

Rais wa Tunisia aweka jeshi mbele kudhibiti janga la COVID-19

Wanajeshi wakilinda mlango wa Bunge, ambapo waandamanaji walikusanyika baada ya hatua ya rais Kais Saied Jumatatu Julai 26, 2021 huko Tunis.
Wanajeshi wakilinda mlango wa Bunge, ambapo waandamanaji walikusanyika baada ya hatua ya rais Kais Saied Jumatatu Julai 26, 2021 huko Tunis. © AP - Hedi Azouz

Tunisia bado inasubiri uteuzi wa waziri mkuu mpya wakati rais Kaïs Saïed alimfuta kazi Hichem Mechichi Jumapili ambaye alikuwa akishikiliwa nafasi hiyo. Jumatano hii, Julai 28, 2021, rais alihutubia taifa akizungumzia maswala kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuunda kitengo cha mgogoro kitakachoratibiwa na jeshi kudhibiti janga la Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Siku chache baada ya kutumia mamlaka yake Jumapili na kutwaa udhibiti wa serikali katika hatua ambayo wapinzani wake wameiita mapinduzi, hatimaye rais Saied amesema lazima nchi yake ikabiliane na mgogoro wa kiafya unaosababishwa na Covid-19.

Amesema anashughulikia hali mbaya ya kiuchumi na janga la COVID-19 nchini humo na kuchunguza tatizo kubwa la ufisadi.

Rais Kaïs Saïed analipa shirika hili haki mpya, haswa ufuatiliaji wa matumizi ya hatua za kiafya, zile za akiba na utekelezaji wa mkakati wa chanjo. Wafanyikazi wa Mgogoro pia watalazimika kutoa maoni na kuripoti kila wiki kwa Mkuu wa Nchi. Uamuzi uliochukuliwa katika hali ngumu ya kiafya. Tunisia ina moja ya viwango vya juu zaidi vya vifo vinavyohusishwa na janga la Covid-19 katika bara la Afrika.

Hii sio mara ya kwanza kwa wanajeshi kushiriki katika sekta ya kiraia. Mamlaka tayari imelitaka jeshi kufanya miradi ya miundombinu au kuleta au kusafirisha bidhaa za msingi katika kutoka maeneo ya mbali ya nchi.

Rais wa Jamhuri alikutana mapema jana na kamanda mkuu wa majeshi na maafisa wakuu wa usalama wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Vikosi vya Wanajeshi. Mkutano ambao ulikusudia kufuatilia maswala ya nchi. Kulingana na Katiba, Kaïs Saïed ndiye mkuu wa majeshi. Rais Saied alimfuta kazi Waziri wa Ulinzi Jumatatu, bila hata hivyo kugusa uongozi wa kijeshi. Mwezi Aprili rais alisema wakati wa kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 65 tangu kuundwa kwa vikosi vya usalama kwamba jeshi lazima "liwahudumie raia na kuonyesha mfano katika utekelezaji wa sheria."