AFRIKA-AFYA

Eritrea bado yasita kuanza kampeni ya chanjo dhidi ya Covid 19

Asmara, mji mkuu wa Eritrea.
Asmara, mji mkuu wa Eritrea. Reuters/Thomas Mukoya

Eritrea ndilo taifa pekee la Afrika ambalo halijaanza kampeni ya kutoa chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, huku Korea Kaskazini ikisalia nyuma kwingineko duniani, wakati huu Tanzania na Burundi zikianzisha kamepni hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wiki hii kampeni ya utoaji chanjo ilianza nchini Tanzania, huku Burundi ikitangaza kukubali chanjo lakini kwa masharti, lakini Eritrea bado imefunga milango yake kwa chanjo katika nchi hiyo.

Mpaka sasa, dozi zaidi ya Bilioni nne za Corona zimetolewa kote duniani, lakini bado kuna utofauti mkubwa kati ya nchi tajiri na masikini kwa mujibu wa takwimu za Benki ya dunia, chanjo ilitolewa kwa mataifa tajiri ni mara 61 zaidi ikilinganishwa na hali ilivyo kwenye mataifa masikini.

Nalo Shirika la afya Duniani WHO linasema ni asilimia 1.6 ya watu barani Afrika ndio waliopata dozi kamili ya chanjo ya kuzuia virusi hivyo.

Taifa la Afrika linaloongoza kwa kutoa chanjo kwa watu wake ni Ushelisheli ambayo asilimia 68 ya watu wamechanjwa, Mauritius asilimia 33 na Morocco asilimia 26.

WHO inasema kupitia Jukwaa la kusambaza chanjo kwa mataifa masikini duniani COVAX, Dozi zaidi ya Milioni 520 zinatarajiwa kufika barani Afrika kufikia mwaka 2021, lakini kuwafikia angalau asilimia 30 ya watu barani Afrika, dozi nyingine 300 zitahitajika.

.