Afrika Kusini: Ujangili wa faru waanza tena baada ya kupungua kutokana na Corona

Faru katika Hifadhi ya kitaifa ya Kruger, Afrika Kusini.
Faru katika Hifadhi ya kitaifa ya Kruger, Afrika Kusini. AFP PHOTO/STEFAN HEUNIS

Ujangili wa faru nchini Afrika Kusini umeongezeka kwa asilimia 50 katika nusu ya kwanza ya mwaka, ikilinganishwa na kipindi hicho cha mwaka 2020, wakati uhalifu huu ulisitishwa na vizuizi vya kiafya dhidi ya janga laCovid-19, wizara ya Mazingira ya Afrika Kusini imetangaza Jumamosi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Katika miezi sita, faru 249 wameuawa kinyume cha sheria katika nchi ambayo ina idadi kubwa ya faru weupe ulimwenguni, dhidi ya 166 katika nusu ya kwanza ya 2020.

"Ingawa idadi hii ni kubwa kuliko idadi ya faru waliouawa kwa ajili ya pembe zao mwaka jana katika kipindi hicho, iko chini kuliko faru 318 waliouawa na wawindaji haramu katika miezi sita ya kwanza ya 2019," wizara hiyo imeongeza.

Mnamo mwaka wa 2020, faru 394 tu waliuawa, idadi ya chini kabisa tangu 2011, kuanzishwa kwa vizuizi vikali katika usafari, hasa za kimataifa, kumezuia uwindaji haramu.

Ujangili wa faru - ambao Hifadhi kubwa ya Kruger ya kitaifa ilikuwa eneo kuu katika nusu ya kwanza ya mwaka - inawahusisha wawindaji haramu nchini humo na mashirika ya uhalifu ya kimataifa wanaosafirisha pembe hizo za thamani, mara nyingi kwenda Asia ambapo bado zinatafutwa.