DRC-USALAMA

DRC: Thelathini na tatu waangamia katika ajali ya barabarani Kibuba

Hali mbaya ya barabara inaelezwa pia kuwa sababu kubwa ya kutokea kwa ajali kama hizi, lakini pia baadhi ya madereva hawana mafunzo ya kutosha na wengine huendesha magari wakiwa walevi.
Hali mbaya ya barabara inaelezwa pia kuwa sababu kubwa ya kutokea kwa ajali kama hizi, lakini pia baadhi ya madereva hawana mafunzo ya kutosha na wengine huendesha magari wakiwa walevi. Eduardo Soteras / AFP

Watu 33 wamepoteza maisha kufuatia ajali ya barabarani baada ya Lori lenye mafuta kugongana uso kwa uso na basi lenye abiria katika kijiji cha Kibuba umbali wa Kilomita 80 kutoka jiji kuu Kinshasa nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wamethibitisha ajali hiyo iliyotokea usiku Jumamosi iliyopita na kusababisha moto mkubwa kuwaka, na kusababisha maafa hayo makubwa.

Kamanda wa Polisi katika eneo hilo Kapten Antoine Pululu amesema idadi kubwa ya miili iliteketezwa na kusababisha ugumu wa kuwatambua watu walioangamia, huku mabaki yao yakizikwa siku ya Jumatatu.

Ajali kama hizi hutokea mara kwa mara nchini DRC sababu kubwa ikiwa ni magari makuu ambayo kwa kiasi kikubwa hayana ubora wa kuwa barabarani.

Pamoja na hilo, hali mbaya ya barabara inaelezwa pia kuwa sababu kubwa ya kutokea kwa ajali kama hizi, lakini pia baadhi ya madereva hawana mafunzo ya kutosha na wengine huendesha magari wakiwa walevi.

Mara ya mwisho kushuhudia ajali kama hii iliyohusisha lori la mafuta ilikuwa ni mwaka 2018 kjaribu na jiji la Kinshasa ambapo watu 53 waliangamia, lakini mwaka 2010 watu wenhgine 230 walipoteza maisha baada ya lori la mafuta kuanguka.