DRC-SIASA

DRC: Uteuzi wa mkuu wa CENI waendelea kuzua sintofahamu, makanisa yashambuliwa

Mjadala kuhusu viongozi wapya wa CENI wagongwa vichwa vya habari DRC.
Mjadala kuhusu viongozi wapya wa CENI wagongwa vichwa vya habari DRC. Caroline Thirion / AFP

Mvutano unaendelea kuhusiana na mchakato wa uteuzi wa wajumbe wa tume ya uchaguzi nchini DRC. Jumatatu hii, makanisa Katoliki na Protestanti yanatarajiwa kuwasiliana ili kuelezea msimamo wao, wakati katika huko Kinshasa na Kasai-Mashariki, makanisa yako chini ya shinikizo la mashambulizi na maandamano.

Matangazo ya kibiashara

Kuchelewa kwa uteuzi wa maafisa wa CENI kunasababishwa na mzozo kati ya madhehebu makubwa mawili ya kikristo, Katoliki na Protestani na mengine sita, ikiwa ni pamoja na Kanisa la Uamsho nchini DRC, juu ya uteuzi wa mwenyekiti wa Ceni. Kati ya madhehebu nane yanayotambuliwa nchini, sita waliamua kutangaza jina la mgombea wao Ijumaa jioni. Lakini kanisa Katoliki na Protestanti wanapinga uhalali wa utaratibu huo.

Je! Uteuzi wa Denis Kadima kwenye nafasi ya mwenyekiti wa CENI ni halali? Kwa kanisa Katoliki na Protestanti, sheria ya hivi karibuni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi, CENI, iko wazi: ni madhehebu tu "yenye uzoefu na utaalam uliothibitishwa katika maswala ya uchaguzi" ndio yanayostahili kupiga kura. Lakini hii ni riwaya iliyowekwa katika Ibara yake ya 10. "Kati ya madhehebu haya sita, ni nani aliye na ujumbe wa uchunguzi au ana ufahamu wa uchaguzi? ",  mmoja wa viongozi madhehebu hayo ya dini amesema.

"Kwa kila uchaguzi mpya, wanamlazimisha mgombea uenyekiti aliye na ukaribu na utawala. Wakati wananchi wa Congo wamekuwa wakiuawa wakitetea demokrasia, hatujawahi kuwasikia wakipinga, ”amebaini pia, akiongeza kuwa kama Cenco kutoka kanisa Katoliki na ECC ya kanisa la Protestanti hawakuwasilisha sheria hii kabla ya Ijumaa, ilikuwa kujaribu kulinda umoja wa jukwaa la madhehebu ya dini ambayo mara hukosolewa.

Makanisa ya Protestanti na Katoliki yanalaani hatari ya utawala kuingilia mchakato wa uteuzi wa mwenyekiti wa CENI. Kwa upande wa  muungano wa upinzani wa Lamuka wa aliyekuwa mgombea urais Martin Fayulu na Waziri Mkuu wa zamani Adolphe Muzito, raia wa Congo lazima wasimame kupinga CENI kuingiliwa kisiasa na wawe tayari kuandamana.