MADAGASCAR-HAKI

Madagascar: Mwendesha mashtaka athibitisha maandalizi ya mapinduzi

Mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Rufaa ya Antananarivo, Berthine Razafiarivony, Agosti 2018.
Mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Rufaa ya Antananarivo, Berthine Razafiarivony, Agosti 2018. © Laure Verneau/RFI

Nchini Madagascar raia wawili kutoka Ufaransa wanakabiliwa na mashitaka ya kujaribu kupindua serikali, licha ya kukanusha madai hayo. Ofisi ya mashitaka ya Antananarivo inasema ina ushahidi.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wiki mbili baada ya kukamatwa kwa raia hao wa Ufaransa, kwa madai ya kutaka kuhatarisha usalama wa nchi, mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Rufaa ya Antananarivo, Berthine Razafiarivony, ametoa hoja kwa waandishi wa habari kuelezea kuhusu maendeleo ya uchunguzi: amethibitisha hasa, kupitia ushahidi uliokusanywa na wachunguzi, kwamba jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali lilikuwa lilipangwa.

Wakati wa upekuzi, wachunguzi walishikilia "bajeti ya mradi wa Apollo 21." Hati hii inaelezea mazingira ambamo mapinduzi yalikuwa wamepangwa: kulikuwa kumeandaliwa mpango wa kina na uliogharimu mapesa mengi kuangamiza wanasiasa watano nchini Madagascar, ikiwa pamoja na Rais wa Jamhuri Andry Rajoelina.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwendesha mashtaka Razafiarivony kuelezea kwa kina ushahidi halisi uliosababisha kukamatwa na kuzuiliwa kwa Paul Rafanoharana na Philippe François. Wawili hao, ambao mmoja ni Mfaransa na mwengine ni Mfaransa mwenye asili ya Madagascar, wote wanaishi Madagascar, walikamatwa Jumanne jioni Julai 20 na kikosi kinachokabiliana na wahalifu. Paul Rafanoharana alikamatwa nyumbani kwake, na Philippe François alikamatwa katika alipokuwa akijiandaa kuondoka nchini humo.

Mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Rufaa ya Antananarivo pia alithibitisha mambo kadhaa yaliyokamatwa na wachunguzi ambayo yalikuwa yamevuja kwenye vymbo vya habari nchini Madagascar: jumla ya pesa karibu euro 200,000, bunduki moja na magari mawili. Kwa jumla, watu ishirini na moja walikamatwa, ikiwa ni pamoja na askari kadhaa, 14 kwa sasa wako chini ya ulinzi, amesema Berthine Razafiarivony.

Uchunguzi unaendelea na umekabidhiwa polisi, kwa ushirikiano na ofisi ya mashtaka ya Antananarivo.