ETHIOPIA-USALAMA

Waasi wa TDF na serikali watupiana lawama kuhusiana na miili inayookotwa

Uharibifu uliosababishwa na mapigano huko Tigray.
Uharibifu uliosababishwa na mapigano huko Tigray. Yasuyoshi CHIBA AFP/File

Miili ya watu 30 imepatikana ikielea mtoni kwenye mpaka wa Sudan na Ethiopia, kwa mujibu wa wakimbizi kutoka mataifa hayo mawili walioona miili hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema, miili hiyo ilipatikana kweye Mto Setit kwa upande wa Sudan lakini nchini Ethiopia unafahamika kwa jina la Tekeze, ambao kwa sasa unadhibitiwa na waasi wa Tigray na wale wa Amhara wanaoshirikiana na serikali ya Ethiopia.

Mmoja wa Madaktari aliyekimbia machafuko katika jimbo la Tigray ameliambia Shirika la Habari la REUTERS kuwa, kwa kipindi cha siku sita zilizopita, amefanikiwa kuzika miili ya watu 10.

Naye mkimbizi kutoka Ethiopia ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema yeye aliona miili tisa ikielemea kwenye maji ya mto huo katika kipindi cha miezi kadhaa sasa ambacho maelfu ya watu kutoka jimbo la Tigray, wamekuwa wakikimbilia nchini Sudan.

Serikali ya Ethiopia kupitia ukurasa wake wa Twitter inasema picha zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na hiyo ni propaganda inayofanywa na waasi wa jimbo la Tigray.