DRC-MAUAJI

Mwanahabari mwingine auawa Mashariki mwa DRC

Jeshi la MONUSCO kwenye mkoa wa Ituri
Jeshi la MONUSCO kwenye mkoa wa Ituri SAMIR TOUNSI / AFP

Mwanahabari mwingine ameuawa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Joël Musavuli Mkurugenzi wa kituo cha redio cha RTCB / Biakato, alipatikana ameuawa pamoja na mke wake  katika kijiji cha Kenya huko Mambasa, Kilomita 100 kutoka mjini Bunia.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa mwanahabari mwenzake, amesema Musavuli na mkewe walivamiwa na watu wenye silaha usiku wa kuamkia Jumamosi wakiwa nyumbani kwao.

Walipigwa na kukatwa kwa mapanga, huku ripoti zikisema Musavuli akipoteza maisha papo  hapo huku mkewe akipoteza maisha Jumamosi asubuhi baada ya kupata majereha mabaya.

Mwanahabari mwenzake, Victor Mauriat, amesema kabla ya kuuawa kwake, Musavuli amekuwa akitishiwa maisha kwa kupigiwa simu na watu wasiofahamika.

Haijafahamika vema, ni mwanahabari huyo alikuwa anatishiwa na baadaye kuuawa.

Hii sio mara ya kwanza kwa mwanahabari kuuawa mashariki mwa DRC, wiki iliyopita, mwanahabari mwingine Héritier Magayane aliuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiofahimika huko Ruthsuru katika mkoa wa Kivu Kaskazini.