DRC-UCHUNGUZI

DRC: Polisi yakamilisha upekuzi nyumbani kwa Jenerali John Numbi

Jzenerali John Numbi (kushoto) na Floribert Chebeya.
Jzenerali John Numbi (kushoto) na Floribert Chebeya. AFP/ Montage

Msako ulioanzishwa na kitengo cha polisi wanasayansi tangu katikati ya juma lililopita umemalizika. Mtu mmoja kutoka kwa familia ya jenerali mtoro anashikiliwa na polisi. Mbali na silaha nyingi za kivita na hati nyingi za serikali zilizogunduliwa, wachunguzi wamepata sare chache tu za polisi zilizofukiwa chini ya ardhi.

Matangazo ya kibiashara

Kuligunduliwa sare nne za polisi zikiwa katika hali nzuri. Sare ambazo inawezekana zilifuliwa kwa mikono kabla ya kufukiwa chini ardhi.

Kitengo cha polisi wanasayansi wanashikilia sare hizo kama vile sampuli za kile kilichoonekana kuwa damu iliyoganda iliyogunduliwa kwenye chumba kidogo kilicho karibu na jiko la nyumba ya Jenerali John Numbi.

Mtu mmoja kutoka familia ya John Numbi alikamatwa kwa uchunguzi, siku hiyo silaha zilipogunduliwa ndani ya nyumba ya jenerali huyo mtoro. Mwanamke huyu anazuiliwai katika jela kuu la Makala, kulingana na vyanzo vya mahakama.

John Numbi anatajwa kama mhusika mkuu wa mauaji ya wanaharakati wa haki za binadamu Floribert Chebeya na Fidèle Bazana katika vituo vya polisi  mwezi Juni 2010. Watu wanne wako kizuizini Kinshasa. Wengine sita wako mafichoni, watatu kati yao wanakiri kushiriki moja kwa moja katika uhalifu huu, kesi yao ambayo hivi karibuni itafunguliwa katika Mahakama Kuu ya Jeshi.