AFRIKA-AFYA

Hati ya kusafiri ya Covid-19 kuanza kutumika Afrika Kusini

Cyril Ramaphosa alihakikisha kuwa chanjo kwa watu wazima ilikuwa sharti la lazima kufungua tena uchumi na kuepusha mlipuko wa nne wa maambukizi.
Cyril Ramaphosa alihakikisha kuwa chanjo kwa watu wazima ilikuwa sharti la lazima kufungua tena uchumi na kuepusha mlipuko wa nne wa maambukizi. GIANLUIGI GUERCIA POOL/AFP

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza nia yake ya kuanza kutumika kwa "Hati ya kusafiri ya Covid-19 ", huku wengi wakipuuzia kuchanjwa dhidi ya Covid-19, katika nchi hii iliyoathiriwa zaidi na virusi vya Corona barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni Jumapili Septemba 12, rais Cyril Ramaphosa alihakikisha kuwa chanjo kwa watu wazima ilikuwa sharti la lazima kufungua tena uchumi na kuepusha mlipuko wa nne wa maambukizi, wakati idadi ya kesi za maabukizi zilipungua kwa kiwango kikubwa nchini Afrika Kusini.

Katika wiki mbili, "tutatoa habari zaidi juu ya mfumo wa hati ya kusafiri ya chanjo ambayo inaweza kutumika kama uthibitisho wa chanjo kwa madhumuni mbalimbali na katika hafla mbalimbali," Cyril Ramaphosa alisema bila kutoa maelezo zaidi. Aliongeza kuwa "kushuka kwa visa vya maambukizi [...] kwa wiki chache zilizopita" ingewezesha, hata hivyo, kulegeza hatua za kudhibiti virusi vya Corona kuanzia Jumatatu.

Muda wa sheria ya kutotoka nje usiku utaongezwa kwa saa moja hadi saa tano usiku na idadi ya watu kukusanyika itaongezwa. Vizuizi dhidi ya ya uuzaji wa pombe pia vitalegezwa, ingawa barakoa zitabaki kuwa lazima katika sehemu zilizo wazi kwa umma.