NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Makumi ya wanafunzi waliotekwa nyara waachiliwa

Wanajeshi wa Nigeria wanapambana na uasi wa kijihadi, na vile vile machafuko ya kikabila na mashambulio mabaya ya magenge ya wahalifu.
Wanajeshi wa Nigeria wanapambana na uasi wa kijihadi, na vile vile machafuko ya kikabila na mashambulio mabaya ya magenge ya wahalifu. AUDU MARTE AFP

Watu wenye silaha wamewaachilia makumi ya wanafunzi waliotekwa nyara mapema mwezi Septemba katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria, kulingana na chanzo cha serikali na video inayoonyesha maafisa na watoto hao, shirika la habari la  AFP limebaini.

Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi hao wa shule ya Kaya waliachiliwa Jumapilihii Septemba 12, baada ya jeshi kuzindua operesheni dhidi ya magenge ya wahalifu ambayo kwa miezi kadha yameongeza utekaji nyara kwa wingi kwa ajili ya fidia kaskazini mwa Nigeria.

Visa vya utekaji nyara wa watu wengi shuleni umeongezeka kaskazini na katikati mwa Nigeria, vitendo vinavyotekelezwa na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu au magenge ya wahalifu wanaojulikana katika eneo hilo kama "majambazi" wanaomba fidia au kuwa na uhusiano na makundi haya yenye silaha.