SUDAN

Mafuriko yaua watu zaidi ya 80 nchini Sudan

Karibu vijiji 50 vimesombwa na maji kusini mwa Sudan, na kusababisha watu 65,000 kukosa makaazi, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Sudan Kusini ambao kambi yao imekumbwa na mafuriko, Umoja wa Mataifa ilisema katika ripoti wiki iliyopita.
Karibu vijiji 50 vimesombwa na maji kusini mwa Sudan, na kusababisha watu 65,000 kukosa makaazi, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Sudan Kusini ambao kambi yao imekumbwa na mafuriko, Umoja wa Mataifa ilisema katika ripoti wiki iliyopita. Ebrahim Hamid / AFP

Mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha yamesababisha vifo vya watu zaidi ya watu 80 nchini Sudan na kuharibu maelfu ya nyumba, afisa wa Sudan amesema Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

"Jumla ya watu 84 wameuawa na wengine 67 wamejeruhiwa katika majimbo 11 ya Sudan tangu kuanza kwa msimu wa mvua," amesema Abdel Jalil Abdelreheem, msemaji wa Baraza la kitaifa la Ulinzi wa raia nchini Sudan.

Vifo hivyo vilitokana na watu kuzama majini, umeme na kuanguka kwa nyumba, ameelezea. Baadhi ya nyumba 8,400 zimedondoka na zaidi ya 27,200 zimeharibiwa kote nchini.

Mvua kubwa hunyesha nchini Sudan kati ya mwezi wa Juni na Oktoba, na nchi hiyo inakabiliwa na mafuriko makubwa kila mwaka ambayo huharibu mali, miundombinu na mazao.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mvua hizi kubwa na mafuriko zimeathiri watu 102,000 tangu mwezi wa Julai.

Karibu vijiji 50 vimesombwa na maji kusini mwa Sudan, na kusababisha watu 65,000 kukosa makaazi, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Sudan Kusini ambao kambi yao imekumbwa na mafuriko, Umoja wa Mataifa ilisema katika ripoti wiki iliyopita.

Mnamo mwaka wa 2020, mvua ziliilazimu mamlaka ya Sudan kutangaza hali ya hatari ya miezi mitatu, na ziliathiri watu wasiopungua 650,000 na kuharibu zaidi ya nyumba 110,000.