MALI-ULINZI

Mamluki wa Urusi kutoka kampuni ya Wagner kutoa mafunzi kwa vikosi vya Mali

Rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, wakati wa akikagua vikosi vya jeshi, Juni 7, 2021 huko Bamako.
Rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, wakati wa akikagua vikosi vya jeshi, Juni 7, 2021 huko Bamako. AFP - ANNIE RISEMBERG

Je? Mamluki wa Urusi wa kampuni ya kibinafsi Wagner hivi karibuni watakuepo nchini Mali? Jibu ni ndio, kulingana na shirika la habari la Uingereza la Reuters, ambalo linasema kuwa mazungumzo kati ya mamlaka ya mpito nchini Mali na kundi la Wagner yanaendelea na "yanakaribia kukamilika".

Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya Wagner tayari lipo barani Afrika, hasa Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo uhalifu linalotekeleza dhidi ya raia umeelezwa na waandishi wa habari, hasa RFI, na mashirika ya haki za binadamu.

Nchini Mali, kwa upande mwingine, itakuwa mara ya kwanza baada ya Ufaransa kukamilisha Operesheni Barkhane na kupunguza wanajeshi wake nchini humo.

Makubaliano ambayo yanajadiliwa hivi sasa, kulingana na shirika la habari la Reuters, yatahusu kutuma mamluki kadhaa au hata mamluki elfu moja wa Urusi kwenda Mali. Kampuni ya Wagner inasemekana kulipwa faranga za CFA bilioni sita - zaidi ya euro milioni tisa - kwa mwezi kwa kufundisha wanajeshi wa Mali na kutoa ulinzi kwa viongozi wengine wakuu. Hakuna ushiriki wa moja kwa moja katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi.

Shirika la habari la Reuters limenukuu vyanzo saba vya kidiplomasia na vya kijeshi, lakini hakuna uthibitisho rasmi, kutoka kwa kampuni ya Wagner au upande wa mamlaka nchini Mali.