DRC: Waandishi wa habari waogopa vitisho na uhasama zaidi uchaguzi unapokaribia
Imechapishwa:
Angalau kesi 110 za mashambulizi ya waandishi wa habari na vyombo vya habari zilirekodiwa mwaka wa 2021, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumanne, Novemba 2 huko Kinshasa na shirika lilislo la kiserikali la JED wakati wa ikiadhimishwa siku ya kupambana na ukatili dhidi ya waandishi wa habari.
Zaidi ya nusu ya matukio haya ya mashambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari huathiri usalama wa kimwili na ni vitisho au hata mauaji, vitendo ambavyo huriporiwa katika mji mkuu na mashariki mwa DRC.
Shirika linalotetea haki za waandishi wa habari, JED, linasema linatiwa wasiwasi hasa kuhusu waandishi wa habari walioko katika mkoa wa Kivu Kaskazini na Ituri, majimbo mawili yalio chini ya sheria ya kijeshi tangu mwezi Mei.
"Inatia wasiwasi sana kwamba ni mikoa miwili tu, ambayo iko chini ya sheria ya kijeshi ambapo kuna ripotiwa idadi kubwa zaidi ya visa vya mauaji, ikiwa ni pamoja na mauaji ya waandishi wa habari," amesema Tshivis Tshivuadi, katibu mkuu wa shirika la JED. Mwaka wanahabari wanee waliuawa. Mwaka jana, waliuawa wanahabari wawili. Jambo la kusikitisha ni kwamba kwa kesi hizi zote hatkuna uchunguzi uliofanyika. "