ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Waziri Mkuu atangaza hali ya hatari nchi nzima

Wapiganaji wa kundi la waasi la TPLF nchini Ethiopia, Juni 2021.
Wapiganaji wa kundi la waasi la TPLF nchini Ethiopia, Juni 2021. AFP - YASUYOSHI CHIBA

Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeendelea kwa mwaka mmoja sasa vimechukua sura mpya tangu mwishoni mwa wiki hii. Waasi katika jimbo la Tigray wameingia katika miji miwili muhimu kaskazini mwa nchi na inaonekana kuwa wanaendelea kusonga mbele dhidi ya jeshi la shirikisho.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii mpya kwa waasi inadhoofisha msimamo wa serikali ya Abiy Ahmed, ambayo sikuya Jumanne, ilitangaza hali ya hatari nchi nzima. Waasi kwa wakati wowote wanaweza kuingia katika mji mkuu wa Addis Ababa.

Wakati waasi wa TPLF wa Tiggy bado wako kilomita 400 kaskazini mwa mji mkuu wa Ethiopia, kusonga kwao mbele katika siku za hivi karibuni kumeweka shinikizo kwa serikali ya shirikisho.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abby Ahmed ametoa wito kwa raia kujilinda dhidi ya waasi. Eneo la Amhara, ambako mapigano yanaripotiwa leo, alitangaza hali ya hatari na kuajiri maelfu ya wanamgambo. Kwa upande wa mji wa Addis Ababa, amewahimiza wakazi kuunda makundi ya kujilinda kukitokea mashambulizi ya TPLF katika mji mkuu huo.

Chama cha Tigrayan People's Liberation Front, TPLF - kimekuwa kikipambana na jeshi la serikali kwa mwaka mzima wameungana na wapiganaji kutoka Oromo -hali inayowapa uwanja mkubwa zaidi wa kuitishia Addis Ababa.

Waziri wa Sheria Gideon Timoteos katika mkutano na vyombo vya habari vya serikali alisema yeyote atakaekiuka sheria ya hatari atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu hadi kumi, kwa makosa kama vile kutoa msaada wa kifedha, vitu au kimaadili kwa makundi ya kigaidi.ukamatwa.