DRC-USALAMA

DRC: Utulivu warejea Bukavu baada ya mapigano ya usiku

Mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, Bukavu, mashariki mwa DRC kwenye ukingo wa Ziwa Kivu.
Mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, Bukavu, mashariki mwa DRC kwenye ukingo wa Ziwa Kivu. © Flickr CC BY SA 2.0 followtheseinstructions

Usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, kundi la washambuliaji ambao hawajajulikana walijaribu kukusanya silaha na risasi kwa kushambulia kambi za jeshi na polisi. Baada ya siku nzima ya sintofahamu kufuatia mapigano hayo kati ya kundi la washambuliaji na jeshi, hali ya utulivu imerejea na shughuli zimerejea tena.

Matangazo ya kibiashara

Katika barabara kuu za jiji, wachuuzi wa mitaani wanajaribu kuangalia muda waliopoteza kwa kuendesha shughuli zao.

"Tunaishi kwa kwa shughuli tunazozifanya kila siku na ilikuwa ngumu kwangu kukaa siku nzima nikiwa sifanyi shughuli yoyote, kwa hivyo nimeamua kuja kufungua biashara yangu. Kwa bahati mbaya hakuna wateja, inaonekana bado wana kiwewe lakini kikubwa ni kwamba utulivu umerejea, na bado naweza kufanya shughuli zangu, " amesema Mireille Ushindi.

Jeshi limetoa wito wa watu kusalia nyumbani hadi hali itakapokuwa shwar baada ya adui kuangamizwa, lakini gavana wa mkoa wa Kivu Kusini Théo Ngwabidje amewatuliza nyoyo raia akisema: "Hali imedhibitiwa. Uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wa shambulio hilo. Ninatoa wito kwa watu wetu watulie, na zaidi ya yote waendelee na shughuli zao za kawaida. Bukavu bado iko chini ya himaya ya serikali. "

Wiki moja iliyopita, mashambulizi mawili yalitokea Kabamba katika eneo la Kabare kaskazini mwa Bukavu, na huko Kaziba kusini magharibi mwa mji mkuu wa Kivu Kusini.