SUDAN-USALAMA

Maandamano dhidi ya mapinduzi Sudan: Orodha ya wafungwa yazidi kuongezeka

Kizuizi lichowekwa kwenye moja ya barabara mjini Khartoum, Sudan, Jumapili hii, Novemba 7, 2021.
Kizuizi lichowekwa kwenye moja ya barabara mjini Khartoum, Sudan, Jumapili hii, Novemba 7, 2021. AP - Marwan Ali

Nchini Sudan, karibu wiki mbili baada ya mapinduzi ya Abdel Fattah al-Burhan, mashirika ya kiraia yalitoa wito kwa raia kususia shughuli za serikali kwa siku mbili zaidi na kufanya mgomo wa jumla Jumapili (Novemba 7).

Matangazo ya kibiashara

Makumi ya walimu waliofanya maandamano ya amani mbele ya wizara ya elimu walitawanywa vibaya. Zaidi ya 80 kati yao walikamatwa, ikiwa ni pamoja na wanaharakati kadhaa wa kamati za upinzani.

Makumi ya walimu waliokuwa wakiandamana mbele ya makao makuu ya Wizara ya Elimu ya Sudan walitawanywa vibaya Jumapili asubuhi mjini Khartoum. Kulingana na chama cha walimu, walimu 87 walikamatwa na mwalimu mmoja alivunjwa mguu katika ghasia hizo. Wanaharakati kadhaa kutoka kamati za upinzani pia walikamatwa. Kwa jumla, polisi na idara ya ujasusi wanawashikilia angalau watu 119, kulingana na wakili.

Katika mji mkuu, maeneo ya Umbada, Burri au Shajara vimelengwa hasa na vikosi vya usalama. Walioshuhudia wanasema baada ya kutawanywa kwa mabomu ya machozi, waandamanaji walifukuzwa na kukkimbilia vichochoroni na baadhi walipigwa risasi za moto.

Katika maeneo mengine ya nchi, huko Atbara kaskazini, au Nyala huko Darfur, na vile vile huko Port-Sudan, mamia ya watu pia waliandamana mitaani siku ya Jumapili. Lakini ikosi vya jeshi na polisi vilikabilian na waandamanaj na kulazimika kutumia nguvu kwa kutawanya maandamano hayo.