Raia wa Afrika Magharibi wapuuzia kupewa chanjo ya Covid-19

Kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19 inapuuziwa nchini Senegal au Benin.
Kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19 inapuuziwa nchini Senegal au Benin. Michele Spatari AFP/File

Chanjo za kuzuia Covid-19 sasa zinapatikana kwa wingi barani Afrika; ni asilimia 5.7 tu ya watu wamekamilisha ratiba kamili ya chanjo, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Nchini Benin au Senegal, kwa mfano, raia wanasita kupewa chanjo.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi mmoja uliopita, Baraza la Mawaziri la Benin liliamua kuendeleza hatua za vizuizi zilizohusishwa na Covid-19, kama kiwango cha chanjo katika ngazi ya kitaifa kitakuwa hakijaboreshwa. Kulingana na takwimu rasmi, nchi hiyo imerekodi chini ya kesi 25,000 zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona kwa jumla, pamoja na vifo 161. Mwanzoni mwa wiki iliyopita, kiwango cha chanjo hakikufikia 4%.

"Bado nina mashaka"

Katika mitaa ya Cotonou, baadhi ya raia bado anasita kupewa chanjo, amebainisha mwandishi wetu maalum huko Cotonou, Magali Lagrange. Watu wachache wanasubiri mbele ya chumba kwenye kituo cha afya, ambapo watapata chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Wagonjwa hupewa hati ya taarifa ... kabla ya kuchomwa sindano. Hervé anakiri kwamba alisi kupwa chanjo: “Niliamua, baada ya muda, kupata chanjo ili kutoa mchango wangu na hasa kwamba nina wazazi wazee tunaoishi nao pamoja. Kwa kile tulichosikia kwenye mitandao ya kijamii, inatufanya kusita kidogo. "

Hiki ni kirusi cha aina gani?

Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji.  Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19.

COVID-19 ni nini?

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.