ECOWAS-USHIRIKIANO

ECOWAS: Wakuu wa majeshi watetea umoja katika vita dhidi ya ugaidi

Mwanajeshi wa Cote d'Ivoire akishika doria katika moja ya mitaa ya Abidjan, Oktoba 22, 2015.
Mwanajeshi wa Cote d'Ivoire akishika doria katika moja ya mitaa ya Abidjan, Oktoba 22, 2015. © AP / Schalk van Zuydam

Abidjan imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 41 wa Kamati ya Wakuu wa majeshi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, wa ECOWAS, tangu Jumatano Novemba 17 hadi Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa hao wa ngazi za juu watajadili kwa pamoja urekebishaji upya wa Operesheni Barkhane na atahri zake zinazoweza kutokea katika kanda hiyo, ambayo bado inakumbwa na mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara.

 

Mtazamo wa pamoja, shughuli za pamoja, kubadilishana taarifa za kiintelejia... Wakuu wa majeshi kutoka ECOWAS (Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi) wanataka kuweka haraka zana za ushirikiano baina ya mataifa ili kukabiliana na tishio la kigaidi linaloelezewa kuwa "linakua". "Vitisho vingi, vya mseto na vya kimataifa" kulingana na Waziri wa Ulinzi wa Cote d'Ivoire, Téné Birahima Ouattara, ambaye ana hofu ya kuondolewa hatua kwa hatua kwa wanajeshi wa Ufaransa katika ukanda wa Sahel:

"Kufafanuliwa upya kwa mkao wa washirika katika Sahel, hasa Barkhane, bila shaka kutaambatana na msukosuko katika kukabiliana na ugaidi katika eneo hili na mbali na eneo hili. Kwa maana hii, kutarajia hali hii mpya ni muhimu kwa ajili ya kuhifadhi udhaifu sawa katika maeneo haya. "

"Tuna uhakika kuwa operesheni za pamoja ndio suluhisho. Tunashughulika vikundi yenye silaha yanayohama kutoka mpaka mmoja hadi mwingine, kulingana na hatua zinazofanywa. Ni dhahiri kwamba, ili kuweza kuwalinda vyema wanajeshi wetu, ni lazima tuchukue hatua kwa pamoja. "

Alipoulizwa kuhusu hatari ya kuongezeka kwa shughuli za makundi ya kigaidi yanayoendesha harakati zao nchini Mali, Burkina Faso na Niger kuelekea nchi za mwambao wa Ghuba ya Guinea, Mkuu wa jeshi la Cote d'Ivoire Lassina Doumbia, amesema hata hivyo anajiamini na bila wasiwasi wowote. Mashambulizi ya hivi majuzi kaskazini mwa Cote d'Ivoire, huko Tehini au Kafolo, hata hivyo, yanahoji waangalizi wanaohofia kwamba msitu wa Comoé, kwenye mpaka na Burkinan, utawezesha uvamizi huo.

“Hapana, hata kidogo, hata kidogo. Wanajeshi wamefunzwa kuendesha vita sehemu zote katika nchi, kila jeshi linafanya mazoezi kulingana na jiografia yake. Cote d'Ivoire ni nchi ya misitu, kwa hiyo msitu wa Comoé hauwezi kuwa eneo gumu kwetu kulifahamu, itakuwa ni jambo lisiloeleweka. Hapana hapana hapana. Ni wazi, Hifadhi ya Comoé inatoa makazi mengi zaidi kwa makundi ya kigaidi yenye silaha, huo ni ukweli. Lakini tunaweza kuwatoa huko pia, kwa sababu tumefunzwa hilo, "amesema Jenerali Lassina Doumbia.

Idadi ya mashambulizi ya kigaidi katika ukanda wa Sahel yaliongezeka kwa 250% kati ya mwaka 2018 na 2020. Raia 2,440 na askari 1,000 waliuawa katika mashambulizi haya. Mnamo 2021, hali ya usalama haijaimarika.