DRC-UCHUMI

Congo Hold-up: Kabila na washirika wake wahusishwa katika ufisadi mkubwa wa fedha

Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila.
Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila. © RFI

Congo Hold-up. Hili ni jina la uchunguzi mpya shirikishi unaotathimini kupotea kwa fedha nyingi za umma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Miongoni mwa wanaodaiwa kuwa wahusika wakuu ni rais wa zamani Joseph Kabila na watu wake wa ndani.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni matokeo ya kazi ya vyombo vya habari 19 washirika wanaojumuika katika muungano wa Ulaya EIC na mashirika matano yaliyobobea, inatoyokana na uchambuzi wa mamilioni ya hati za benki na miamala ambayo imevuja kutoka benki ya Afrika: BGFI.

Ukiwa na hati za benki milioni 3.5 na miamala zaidi, uchunguzi wa Congo Hold-up unatokana na kile ambacho hadi sasa, ni uvujaji mkubwa zaidi kutoka bara la Afrika. Unafichua jinsi benki ya biashara, BGFI, ilivyotumika kupora fedha za umma na maliasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Uchunguzi huo unafichua, kwa mara ya kwanza, majina ya wale ambao walishiriki kwa kiasi kikubwa katika kupotea huku kwa utajiri wa nchi miongoni mwa nchi maskini duniani. Nchini DRC leo, zaidi ya 70% ya wakazi wanaishi chini ya dola mbili kwa siku.

Makao makuu ya BGFIBank mjini Kinshasa.
Makao makuu ya BGFIBank mjini Kinshasa. © PPLAAF

Joseph Kabila alengwa

Uchunguzi wa Congo Hold-up umewataja watu kutoka familia ya rais wa zamani Joseph Kabila (2001-2013) na baadhi ya washirika wake wa karibu kuwa ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa wahusika wakuu wa ufisadi huu. Kati ya mwaka 2013 na 2018, kwa msaada wa BGFI, waliweza kuchukuwa angalau dola Milioni 138 kutoka hazina ya serikali. Hii ni sawa na miaka 250,000 ya mshahara wa wastani nchini DRC.

Pia imegundulika kuwa zaidi ya dola milioni 100 za ziada ziliwekwa kwenye akaunti za watu wa familia za ndani za washirika wa karibu wa rais wa zamani Joseph Kabila bila hata hivyo asili ya fedha hizi kuweza kujulikana. Dola milioni thelathini na tatu, pesa taslimu, zilitolewa, na milioni 72 zilitoka kwa akaunti ya BGFI katika Benki Kuu ya DRC (BCC).

Historia ya kundi la BGFI imekumbwa na kashfa za ufisadi na ufujaji wa pesa zinazohusisha watawala wa Kiafrika na makampuni ya Ulaya. Benki hii, iliyo na historia mbaya ya kuhusishwa na "bidhaa zilizopatikana kwa njia mbaya."