RFI-KIFO

Mwanahabari wa RFI Kifaransa Stanislas Ndayishimiye afariki dunia

Stanislas Ndayishimiye
Stanislas Ndayishimiye © @ RFI Mandenkan

Radio France International, kwa masikitiko makubwa inatangaza kifo cha mwanabahari wake Stanislas Ndayishimiye, ambaye amekuwa akifanya kazi katika idara ya uchumi katika Idhaa ya Kifaransa.

Matangazo ya kibiashara

Kifo chake kimejiri Ijumaa usiku kuamkia Jumamosi, baada ya kulazwa hospitalini kwa muda wa mwezi mmoja.

Ndayishimiye aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59, alianza kazi ya uanahabari katika taifa lake alikozaliwa la Burundi, wakati huo akifanya kazi na Shirika la Taifa, lakini pia akishirikiana na RFI.

Hata hivyo, mwaka 1993 alikimbilia nchini Ufaransa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake, na kuendelea kushirikiana na RFI.

Mwaka 1999 aliajiriwa na RFI Idhaa ya Afrika, na baadaye kati ya mwaka 2011 hadi 2014 alikuwa ripota wa Idhaa hii jijini Abidjan nchini Cote Dvoire, na aliporejea jijini Paris nchini Ufaransa, alijiunga na kitengo cha biashara.

Uongozi wa RFI unatoa salamu za pole kwa mke wake na wanawe wawili, wanahabari wenzake, marafiki na wote waliomfahamu wakati wa uhai wake.