LIBANON-SIASA

Jan Kubis ajiuzulu kwenye wadhifa wake kama mjumbe wa UN nchini Libya

Kitengo cha mawasiliano cha UN hakijatoa taarifa yoyote kuhusiana na kujiuzulu kwa Jan Kubis.
Kitengo cha mawasiliano cha UN hakijatoa taarifa yoyote kuhusiana na kujiuzulu kwa Jan Kubis. STR AFP/File

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Jan Kubis, amejiuzulu wadhifa wake mwaka mmoja tu baada ya kuteuliwa, wakati huu Libya ikijitaryasha kwa uchaguzi wa disemba 24 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kubis amejiuzulu mwezi moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Libya, uchaguzi unaotarajiwa kumaliza mzozo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 10, vianzo vya habari vikidai huenda amejiuzulu kutokana na kile ametaja kukosa uungaji mkono wa kutosha kutoka kwa umoja wa mataifa.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa hivi majuzi lilikosa kuelewana, kuhusu iwapo mjumbe wake wa kisiasa anaweza kuhamishwa kutoka Geneva hadi Tripoli, Kubis akionekana kupinga hatua hiyo.

Kitengo cha mawasiliano cha Umojawa mataifa hakijatoa taarifa yoyote kuhusiana na kujiuzulu kwa Kubis.

Kujiuzulu kwake kunajiri siku moja baada ya tume ya uchaguzi ya Libya, kufunga maombi ya wanaotaka kuwania urais, kwenye uchaguzi wa Desemba 24, ambapo wagombea 98, wamewasilisha maombi yao kwa tume hiyo, wakiwemo wanawake wawili.