Ujerumani

Maradhi yanayosababishwa na matango hayajawahi kushuhudiwa

Matango ni aina ya matunda ambayo yana vitamini nyingi.
Matango ni aina ya matunda ambayo yana vitamini nyingi. © REUTERS

Watalaam wa afya nchini Ujerumani wanasema kuwa maradhi yanayosababishwa na matango ni bakteria wapya, na wanaweza kuathiri maini na damu ya mtumiaji.Backteria hao ambao wamezuka huko Ujerumani na Sweden hadi sasa wamesababisha vifo vya takriban watu 18 na zaidi ya watu 1500 wameathiriwa na backteria hao baada ya kula matango hayo.

Matangazo ya kibiashara

Waatam wa kiafya kutoka Shirika la Afya Duniani WHO wanasema kuwa hali hiyo haijawahi kushudiwa, huku wanasayansi kutoka China wakidai kuwa bakteria hao ni hatari sana na wana sumu ambayo pia inaweza kusambazwa kwa haraka.
Aidha, Serikali ya Uhispania imepinga taarifa kutoka Ujerumani, inayodai kuwa matangao hayo, yametoka nchini humo.

Bakteria hao wamesababisha idadi kubwa ya watu kuharisha nchini Ujerumani na wataalam wa kiafya wameonya wasafiri wanaoelekea Ujerumani, kutokula matango hayo kwani yanaweza hatarisha usalama wa maisha yao.