SOMALIA

AU kukutana Jumanne ijayo, kujadili namna ya kukabiliana na ukame

Mungu awajaalie watoto hawa kupata nafuu mapema.
Mungu awajaalie watoto hawa kupata nafuu mapema. Reuters

Mashirika ya misaada yameendeleza juhudi za kuwapatia chakula, waathirika wa baa la njaa nchini Somalia na Umoja wa Afrika, umepanga kukutana jijini Adiss Ababa kujadili namna ya kukabiliana na ukame. Hayo yanajiri wakati ndege za Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula (WFP) zikionekana mjini Mogadishu na kwingineko, zikisambaza chakula kwa maelfu ya watoto, walioko katika hatari kubwa.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu zinaonesha kuna maelfu ya watoto wenye utapiamlo, mjini Doolow, kusini mwa Somalia.
 

Akithibitisha taarifa hizo, msemaji wa Mpango wa Chakula Duniani, David Orr amesema jumla ya ndege sita zimeshasafirisha chakule chenye virutubisho vingi kwa wananchi hao.
 

Na Baba Mtakatifu Benedict XVI, ameiomba dunia isijitenge na janga la njaa, linaloshuhudiwa katika pembe ya Afrika.
 

Akiwahutubia maelfu ya mahujaji waliokusanyika Castel Gandolfo, jijini Rome, Italia, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki ametoa wito huo, siku chache kabla ya Umoja wa Afrika, kukutana tarehe tisa, Agosti.