Ugonjwa wa Surua (Measles) Athari na Tiba zake
Imechapishwa:
Sauti 10:31
Surua ni mojawapo ya magonjwa ya kuambukiza yanayotisha kwa binadamu.Ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya “Morbillivurus paramyxvirus” vinavyoenea kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,na huenezwa kwa njia ya hewa pale mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya. Ugonjwa huuhuathiri watu wa rika zote,licha watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndio huathirika zaidi,Makala ya Siha Njema juma hili itangazia juu ya chanzo na dalili za ugonjwa huu wa Surua