CANADA, MAJANGA

Canada: moto wapungua Fort McMurray

Magari yatymiwa katika zoezi la uokoaji wa wakazi wa Fort McMurray Mei 6 2016.
Magari yatymiwa katika zoezi la uokoaji wa wakazi wa Fort McMurray Mei 6 2016. REUTERS/Mark Blinch

Baada ya hofu kutanda kwa siku kadhaa, matumaini yamerudi katika mji wa Fort McMurray ambapo moto mkubwa ulioibuka katika eneo hilo umeanza kupungua na kutokua tena kitisho kwa mitambo ya mafuta.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo zoezi la kuwaokoa wakazi wa mji huo limefanikiwa. Wakazi wa mji wa Fort McMurray wameonyesha furaha yao baada ya kupata taarifa kuwa moto huo sasa umeanza kupungua.

Waziri Mkuu wa Alberta, Rachel NOTLEY, anatarajiwa kuwasili Jumatatu Mei 9 katika mji wa Fort McMurray. Atatembelea kwa mara ya kwanza eneo hilo lililoteketea kwa moto na kupewa taarifa kwa ufupi kuhusu hasara iliyosababishwa na moto huo wa ajabu. Jumapili, moto ulionekana kuanza kupungua ikilinganishwa na jinsi ilivyokua imetabiriwa. Kwa sasa sehemu inayopima kilomita mraba 1610 imeteketea kwa moto, na mitambo ya mafuta iliyopo kaskazini mwa mji huo haikabiliwi tena na kitisho cha kushambuliwa kwa moto. Watu 80 000 ambao walikimbia eneo hilo wameelezea furaha yao. Hapakua na majeruhi wakati wa zoezi la uokoaji ambalo lilifanyika kwa muda wa siku mbili, ispokuatu watu wawili waliopata ajali ya barabarani.

Kwa siku mbili mfululizo, magari, misafara, malori yaliyokua yakiwasafirisha wakazi 80,000 yalisababisha foleni katika barabara kuu moja tu inayounganisha mji wa Fort McMurray na maeneo yanayosalia ya Alberta. Baadhi walikimbilia kaskazini, wengine upande wa kusini, wakati mwingine wakivuka kuta za moto, wakati ambapo wimbi la majivu lilikua likidondoka kwenye magari yao gari yao.

Mji wa Fort McMurray unapatikana karibu na msitu, kilomita mia kadhaa kutoka mji wa karibu. Wakazi wa mji huo wamekua wakipewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, na wanajua jinsi gani ya kukabiliana na majanga kama hayo iwapo yanatokea.