ZIMBABWE-MAZINGIRA

Zimbabwe kuwang'oa faru pembe zao kwa kuwalinda

Faru mweupe.
Faru mweupe. REUTERS/Ken Bohn/San Diego Zoo

Shirika linalohusika na ulinzi wa wanyamapori (Aware Trust) linasema kuwa Serikali ya Zimbabwe itawang'oa pembe faru wote nchini Zimbabwe ili kuzuia ujangili.

Matangazo ya kibiashara

Mradi uhuu naratibiwa na Mamlaka ya Hifadhi na usimamizi wa wanyamapori nchini Zimbabw.

Lengo ni kuelezea majangili kwamba hakuna pembe za faru nchini Zimbabwe.

Baadhi ya faru 50 waliuawa mwaka jana, kwa jumla ya faru 700 waishio Zimbabwe.

Kuna marufuku ya kimataifa katika biashara ya pembe za faru lakini ujangili wa faru na tembo umeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.