HAITI-KIMBUNGA

Kimbunga kikali chapiga pwani ya magharibi mwa Haiti

Nchi ya Haiti imeendelea kukumbwa na kimbunga kikali. Kimbunga hiki kinachojulikana kwa jina la Matthew kinaendelea kwa kasi kikielekea eneo la kaskazini. Kimbunga hiki kilipiga Jumanne hii mchana pwani ya Haiti.

Mitaa ya eneo la Cite Soleil kitongoji cha mji wa  Port-au-Prince, ikikumbwa na mafuriko Jumanne, Oktoba 4, 2016.
Mitaa ya eneo la Cite Soleil kitongoji cha mji wa Port-au-Prince, ikikumbwa na mafuriko Jumanne, Oktoba 4, 2016. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Upepo wenye kasi za kilomita 220 kwa saa pamoja na mvua nyingi vilishuhudiwa katika pwani ya kusini mwa Haiti. Kulingana na makadirio ya muda, kimbuga Matthew kimesababisha watu saba kupoteza maisha . Na kwa sasa eneo la kaskazini magharibi la limeanza kuvamiwa.

Kwa sasa mvua inanyesha kwa wingi magharibi mwa nchi na barabara kuu, hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince na Léogâne, imeanza kukumbwa na mafuriko.

Katika mji mkuu, watu wamekua na wasiwasi kuhusu mto Grise. Mto huo umekua ukisababisha upepo mkali na maafisa wa Idara za dharura wameshindwa kuwakinaisha wakazi wa mji huo. Watu wengi wamekua wakijielekeza kwenye mto huo ili kushuhudia hali hiyo ya kutisha, huku wengine wakicheka wanaposukumwa na upepo mkali unaosababidshwa na mawimbi ya mto huo. Na wale ambao wanaishi katika nyumba hatari bado wanasita kuondoka katika maeneo hayo.

Mkoa unaoathirika zaidi nchini Haiti ni Grand Sud, hasa karibu na maeneo ya Jeremie na Les Cayes. Kiwango cha mafuriko na uharibifu ni kikubwa, lakini kwa sasa, ni vigumu kujua hali halisi katika eneo lote la kusini mwa nchi.

Bado mpaka sasa haijafahamika kiwango cha uharibifu wa kimbunga hicho nchini Haiti, lakini nyumba nyingi zimebomolewa, huku barabara zikiwa hazipitiki kutokana na miti iliyoanguka pamoja na mafuriko.

Kimbunga Matthew kinatarajiwa kupiga nchini Cuba katika masaa machache kabla ya kkuelekea katika jimbo la Florida. Katika jimbo la Florida ambapo mkutano wa hadhara wa Hillary Clinton ulifutwa kwa sababu ya hatari ya kimbuga hiki.