NASA-DUNIA-MWEZI

Mwezi kuwa mkubwa siku ya Jumatatu

Saa 8:22 saa za Afrika Mashariki sawa na saa 5:22 saa za kimataifa, Mwezi utakua kwenye kilomita 356.509 na dunia.
Saa 8:22 saa za Afrika Mashariki sawa na saa 5:22 saa za kimataifa, Mwezi utakua kwenye kilomita 356.509 na dunia. AFP PHOTO / LUIS ROBAYO

Kwa mujibu wa wataalamu wa Shirika la anga la Marekani la NASA, Jumatatu Novemba 14 Mwezi utakua mkubwa, na mpana, na utashuka na kuwa karibu zaidi na Dunia hali ambayo ni ya kipekee kwa karibu miaka 70 iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

NASA inasema Mwezi huo utaonekana mkubwa kuliko unavyokua kawaida. Tukio hili ahlijawahi kuonekana tangu mwezi Januari 1948 na tukio kama hili litatokea tena mwezi Novemba 2034. Wakati wa usiku, Mwezi utaonekana mkubwa na kuang'ara kuliko unavyokua kawaida.

Hali hii inatokana na matukio mawili yanayoambatana angani: awamu ya Mwezi mkubwa, ambayo hufanyika kila baada ya siku 28, itatokea tu wakati mmoja ambapo nyota ambayo mhimili wake ni laini, itakuwa karibu na Dunia.

Mwezi utafikia hatua yake yakaribu kabisa na Dunia saa 8:22 saa za Afrika Mashariki (sawa na 5:22 saa za kimataifa). Wakati huo mwezi utakuwa "tu" kwenye kilomita 356 509, wakati ambapo umbali wake wa wastani nikilomita 384 400. Utaonekana mkubwa na mpana saa 10:52 saa za Afrika Mashariki (sawa na saa 7:52 saa za kimataifa). Usiku, "Mwezi wa kipekee" utaonekana kwa jicho mahali popote duniani. Angalau kama hali ya hewa itaruhu.