MOROCCO-COP 22

COP 22: Mohammed VI awasihi viongozi wenzake

Mfalme wa Morocco Mohammed VI amewasihi viongozi wenzake barani Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kuwa na kauli moja kwa kabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Katika mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP22), viongozi zaidi ya thelathini kutoka nchi za Afrika walikutana, Jumatano, Novemba 16, 2016.
Katika mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP22), viongozi zaidi ya thelathini kutoka nchi za Afrika walikutana, Jumatano, Novemba 16, 2016. REUTERS/Youssef Boudlal
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Afrika wanapaswa kuzungumza kwa kauli moja, huu ni ujumbe wa Mfalme wa Morocco Mohammed Vi alioutoa Jumatano wiki hii.

"Nimepata fursa ya kuwakaribisha kwa mkutano huu ili bara letu liwajibike kwa kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi . Napendekeza tuwajibike kulipa nafasi bara letu, Afrika ambayo itatumia rasilimali zake kwa kuheshimu usawa wa kimazingira na kijamii. Hata hivyo, itakumbukwa kwamba muda wa ukoloni umepitwa na wakati, uamuzi unaotolewa kwa shinikizo hauwezi kuzaa matunda. Je tunaweza kusema kuwa wahusika wamekosa nguvu, ahadi au nia njema, lakini inafikia wanakosa uwezo," amesema Mfalme Mohammed VI.

Uwezo ulioahidiwa mwaka jana mjini Paris, lakini bado haupo na kwamba Afrika inaendelea kudai. Kwa mujibu wa Rais wa Senegal Macky Sall, sio tu sheria kuhusu hali ya hewa, lakini pia kwa ajili ya usalama wa chakula katika bara hili. "Mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika yanaathiri hasa sekta muhimu za bara hilo. Ambazo ni: kilimo, ufugaji, uvuvi na mazingira ikiwa ni pamoja na ukataji miti na mmomonyoko wa ardhi ".

Baada ya mkutano huo, wakuu wa nchi hatimaye walikubaliana mambo matatu: kupambana na ukataji miti, kulinda maeneo yanayoshambuliwa kimazingira na kuweka sawa eneo la Bonde la Congo.

Jitihada zimeongezwa katika suala la mabadiliko ya tabia nchi. Nchini Burkina Faso, kwa mfano, shirika lisilo la kiserikali la "Water Aid" linawaelekeza wakazi wa kijiji cha Sablogo katika usimamizi wao wa maji. Wataalamu wa masuala ya mvua wamekua wakipima kiwango cha maji kila baada ya kipindi cha mvua.