AFRIKA KUSINI-MAJI

Afrika kusini: vikwazo dhidi ya wale ambao hutumia maji mengi mno

Manispaa ya mji wa Pretoria imenunua mitambo 3 000 ya kuhesabi kiawango cha maji na imetishia kuiweka katika baadhi ya vitongoji ambapo hutumia maji mengi mno.
Manispaa ya mji wa Pretoria imenunua mitambo 3 000 ya kuhesabi kiawango cha maji na imetishia kuiweka katika baadhi ya vitongoji ambapo hutumia maji mengi mno. Petrus Potgieter/CC/Wikimedia Commons

Wakati mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP 22) ukifikia kileleni, manispaa katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini zimeanza kuwachukulia vikwazo wale ambao hutumia maji mengi mno.

Matangazo ya kibiashara

Meya wa mji wa Pretoria yuko mbioni kuweka mitambo ya kuhesabu kiwango cha matumizi ya maji kwa familia ambazo hutumia maji mengi mno. Afrika Kusini inakabiliwa na uhaba wa maji safi. Ni miaka itatau sasa ya ukame na kiwango cha hifadhi ya maji ni kiko chini nchini kote.

Kiongozi huyo amenunua mitambo 3 000 ya kuhesabu kiwango cha matumizi ya maji na ametishia kuweka mitambo hiyo katika baadhi ya maeneo ambapo hutumia maji mengi mno. Tangu miezi 2 manispaa ya jiji la Pretoria imeweka vikwazo juu ya matumizi ya maji. Lakini licha ya vikwazo hivyo, familia nyingi katika vitongoji kadhaa hutumia maji mengi mno.

"Wale ambao mara kwa mara hukiuka vikwazo watapaswa kutumia mitambo ya kuhesabu kiwango cha matumizi ya maji, ni wale ambao hujaza visma vyao vya kuogelea, wale ambao wamekua wakiendelea kumwagilia bustani zao mcahan kutwa, " amesema Solly Msimanga, Meya wa mji Pretoria.

Manispaa ya jiji la Pretoria tayari imetoza faini kwa watu zaidi ya arobaini wanaotumia maji mengi mno. Lakini Jacques Laubscher, Mtaalamu wa masuala ya maji, amesema tatizo la msingi ni tabia za watu. "Kama tabia za watu katika mahusiano ya maji haizitabadilika, hatua hizi zitakua hazina umuhimu wowote. Lazima kuwepo na mabadiliko makubwa kwa watu wanaotumia maji, " amesema Bw Laubscher.

Kwa mujibu wa Jacques Laubscher, kinachotakiwa kufanywa kwa haraka ni mabadiliko ya tabia, kurekebisha miundombinu iliyozeeka na hasa kuanza tena kutoa maji kwa mgao.