EBOLA-AFYA

Ebola-Utafiti: watu walioambukizwa lakini hawana dalili za ugonjwa

Kiijana huyo kutoka Liberia akipewa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola katika hospitali ya Redemption ya mji wa Monrovia.
Kiijana huyo kutoka Liberia akipewa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola katika hospitali ya Redemption ya mji wa Monrovia. RFI/Sébastien Nemeth

Mwaka mmoja baada ya kukoma rasmi kwa ugonjwa wa Ebola katika Afrika Magharibi, baadhi ya watu, ingawa wameambukizwa virusi vya ugonjwa juo katika kijiji cha Sukudu nchini Sierra Leone, hawajawahi kuwa na dalili za ugonjwa, kulingana na utafiti iliyochapishwa Jumanne Novemba 15 katika jarida la PLOS Negleted Tropical Diseases.

Matangazo ya kibiashara

Madhumuni ya utafiti huu, uliyochapishwa Novemba 15, ni kujua uwiano wa wanakijiji walioambukizwa virusi vya Ebola na ambao hawajawahi kuwa wagonjwa. Wanasayansi wamegundua watu 14 walioambukizwa na ambao hawana dalili za uginjwa kwa jumla ya wagonjwa 187.

Virusi vya Ebola vinavyosababisha homa kali na kutokwa na damu na inaambukia kwa njia ya damu au maji maji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa. Dalili hizo zinaweza kuwa homa, kutokwa na damu, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, upele, kutapika, kuharisha, ugumu wa kupumua au kumeza.

Tahmini yenye kuaminika

Watafiti wanabaini kuwa sehemu ya janga haijawahi kugunduliwa. "Lengo la utafiti huu ni kujua uwiano gani wa watu katika maeneo ambapo kuna Ebola hawakuwahi kuwa na dalili za ugonjwa. Hivyo ni jambo la kawaida kuwa katika kijiji ambapo kulikuwa na Ebola. Watafiti hao wanaona 7.5%, tafiti nyingine zinagundua 6% au 5% , idadi hii imekua ikitofautiana sana, " ameeleza Profesa Yazdan Yazdanpanah, mtafiti katika INSERM.

Ili kupta matokeo haya, wanasayansi "walitumia damu".

Zaidi ya matukio 28 000 ya maambukizi yalihesabiwa wakati wa janga hili katika Afrika Magharibi, janga kubwa na lililodumu muda mrefu katika historia ambalo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 11 000.