UKIMWI-AFYA

Siku ya Kimataifa dhidi ya Ukimwi: kuzidisha jitihada na uwezo

Vipimo vya damu bado ni hatua ya kwanza ili kuzuia virusi vya Ukimwi kuviambukiza wengine
Vipimo vya damu bado ni hatua ya kwanza ili kuzuia virusi vya Ukimwi kuviambukiza wengine Flickr, andrew_stevens_h

Tarehe 1 Desemba kila mwaka, wanaharakati katika mapambano dhidi ya Ukimwi wanahamasisha kuhusu ugonwa huo unaoangamiza familia mbalimbali ulimwenguni.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, kampeni za kuhamasisha na mapendekezo ya wataalamu, janga hili linaweza kutokomezwa mara moja kama kutakua na juhudi na uwezo. Lakini karibu nusu ya watu wanaoishi na VVU duniani wanapuuzia mbali hoja hiyo.

Katika mwaka 2015, watu wanne wenye virusi vya ukimwi kati ya 10 hawa kuwa wanajua hali ya afya, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema. Katika Umoja wa Ulaya, mtu mmoja mwenye VVU kati ya 7 apuuzia hali yake ya afya, takwimu ambayo inatia waswasi Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa sababu nusu ya kesi zilizofanyiwa vipimo matokeo yake hutolewa baada ya kuchelewa, baada ya miaka 4.

Katika nchi 28 ikiwa ni pamoja na Iceland, Liechtenstein na Norway, maambukizi kwa wanaume waliojihusisha na uesharati na wanaume wenzao yanaendelea kukua. Lakini nchini Urusi, maambukizio ya ukimwi yamevunja rekodi na kufikia, 64%, lakini sasa njia ya kwanza ya maambukizi hupatikana miongoni mwa watu wa jinsi tofauti na si miongoni mwa mashoga tofauti na nchi hizi 28. HIV inatia wasiwasi kwa afya ya umma wa ukanda huu wa Ulaya ya Mashariki ikiwa ni pamoja na Ukraine, Belarus, Estonia, Moldova, Latvia na Georgia.

Vipimo vya damu bado ni hatua ya kwanza ili kuzuia virusi vya Ukimwi kuviambukiza wengine. Hata hivyo, mamilioni ya watu bado hawawezi kupata matibabu muhimu, amelaumu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO. Kila nchi inahitaji na kutekeleza mipango ya utekelezaji ili kuboresha huduma za kupima na kuzuia kusambaa kwa virusi vya Ukimwi.

Duniani kote, 80% ya takriban watu milioni 6 kwaliopimwa VVU sasa wanahudumiwa kimatibabu ili kupunguza makali ya Ukimwi.