AFRIKA-UCHUMI-MAZINGIRA

Nchi 5 za Afrika zapiga marufuku mafuta machafu

Umoja wa Mataifa unabaini kwamba mpango wa kuzuia mafuta machafu utasaidia zaidi ya watu milioni 250 kupumua hewa salama na safi.
Umoja wa Mataifa unabaini kwamba mpango wa kuzuia mafuta machafu utasaidia zaidi ya watu milioni 250 kupumua hewa salama na safi. AFP

Nigeria, Benin, Togo, Ghana na Cote d'Ivoire wameamua kuacha kuagiza "mafuta machafu" kutoka Ulaya. Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Mazingira linabaini kwamba mpango huu utasaidia zaidi ya watu milioni 250 kupumua hewa salama na safi.

Matangazo ya kibiashara

Nchi za Nigeria, Benin, Togo, Ghana na Cote d'Ivoire, ambazo zote ni kutoka Afrika Magharibi zimechukua uamuzi huo kwa minajili ya kukabiliana na uchafuzi wa Mazingira.

"Afrika Magharibi imetuma ujumbe mkali ikisema haikubali mafuta machafu ya Ulaya," amesema Erik Solheim, mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Mazingira.

Ripoti ya hivi karibuni iligundua kuwa makampuni ya Ulaya yameku ayakitumia taratibu zisizokuwa sahihi katika Afrika Magharibi kwa kuuza nishati kwa kiwango cha juu kabisa.

Chembe za mafuta zinazotolewa na injini ya dizeli zinachukuliwa kama changamoto kubwa ya uchafuzi wa hewa na kuwekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama moja ya athari kuu kiafya ulimwenguni.

Chembe hizi zinahusishwa na ugonjwa wa moyo, kansa ya mapafu na matatizo ya kupumua.