INDONESIA-HALI YA HEWA

Watu wengi wafariki kufuatia tetemeko la ardhi nchini Indonesia

Katika mitaa ya eneo la Banda wilayani Aceh ambapo tetemeko la ardhi limewaua watu wengi.
Katika mitaa ya eneo la Banda wilayani Aceh ambapo tetemeko la ardhi limewaua watu wengi. Marie Normand

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia na kuua watu zaidi ya 24 na kusababisha uharibifu mkubwa. Indonesia ni moja ya nchi zinazokabilia na majanga mbambali ikiwa ni pamoja na vimbunga barani Asia.

Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo la nguvu ya 6.4 kwenye vipimo vya Richter lilitokea karibu na mji wa Sigli katika kisiwa cha Sumatra. Majumba mengi yameporomoka kufuatia tetemeko hilo.

Taasisi ya Jiolojia ya Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani hiyo saa 11:03 asubuhi saa za Indonesia ( sawa na saa 4:03 usiku saa za kimataifa) katika kina cha 17.2 kilomita (maili 11) chini ya ardhi.

Maafisa wanasema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka, na mpaka sasa shughuli ya uokozi inaendelea, idara ya huduma za dharura imesema.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia limewatuliza nyoyo viongozi na wananchi wa taifa hilo kuwa hakuna tichio la ktokea kimbunga chochote katika eneo hilo au katika maeneo mengine ya nchi.

Wilaya ya Pidie Jaya, ndio ambayo imeathirika zaidi na tetemeko hilo, huku maafisa wakisem akuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Mwaka 2004, mkoa wa Aceh uliathiriwa sana na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa lililoanzia baharini. Watu 120,000 waliuawa mkoani humo kufuatia tetemeo hilo.