WHO-AFYA

WHO: Ugonjwa wa moyo wakithiri Afrika

Kipimo cha mapigo ya moyo.
Kipimo cha mapigo ya moyo. Getty Images/Mutlu Kurtbas

Shinikizo la damu, ni ugonjwa ambao umekithiri barani Afrika, Asilimia zaidi ya 10 ya Waafrika wanakabiliwa na ugonjwa huo, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO).kupuuza Afrika

Matangazo ya kibiashara

Kufanya mazoezi ya kila aina, kula matunda angalau matano na mboga kwa siku, kutotumia tumbaku au sigara na pombe, ni moja ya njia za kupambana na ugonjwa wa moyo, kansa au kisukari.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), robo ya watu wazima kutoka nusu ya nchi Afrika zilizofanyiwa utafiti wana angalau sababu tatu za hatari zinazoongeza uwezekano wa kuwa na moja au zaidi ya magonjwa hayo wakati wa maisha yao.

Ripoti hiyo ya WHO inaonyesha kuwa wanawake wa Afrika wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa haya.

Wakati ambapo matumizi ya tumbaku au sigara na pombe yako kiwango cha chini barani Afrika kuliko sehemu zingine duniani, shinikizo la damu iko katika kiwango cha juu zaidi duniani, na kuathiri karibu nusu ya ya watu wazima.

Kwa mujibu wa WHO, kiwango hicho kinatisha kwa sababu ugonjwa huo unaathiri pole pole na mara nyingi unagunduliwa baada ya miaka kadhaa.

Bara la Afrika pia ni mahali pekee watu wanakabiliwa na utapiamlo na fetma.

Hata hivyo matatizo yote haya ya afya yanaweza kuzuiwa kwa kula vizuri, kunywa kwa kiasi na kufanya mazoezi.

Kama tahadhari hizi hazizingatiwi, hali hii inaweza kupelekea serikali kugharimu mabilioni ya pesa katika matibabu ya magonjwa haya.