MAREKANI-HALI YA HEWA-TRUMP

Hali ya Hewa: Jumuiya ya kimataifa yapinga uamuzi wa Trump

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) ni mmoja kati ya viongozi wa dunia waliokosoa uamuzi wa Donald Trump.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) ni mmoja kati ya viongozi wa dunia waliokosoa uamuzi wa Donald Trump. REUTERS/Jonathan Ernst

Viongozi mbalimbali wa dunia wamekerwa na hatua ya rais Trump kuiondoa Marekani katika mkataba huo uliotiliwa saini na mataifa 187 jijini Paris, nchini Ufaransa mwaka 2015.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelaani hatua hiyo ya rais Trump na kusisitiza kuwa Ufaransa itatekeleza mkataba huo ili kufanikisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Aidha amesema, utekelezwaji wake ni muhimu kwa manufaa ya dunia katika siku zijazo. China imesema hatua ya Marekani inarejesha nyuma juhudi za kupambana na ongezeko la joto duniani.

Maafisa wa juu wa serikali za Ujerumani na Italia nao wameshtumu hatua ya rais Trump na kusema hawapo tayari kurejea tena katika meza nyingine ya mazungumzo kama anavyopendeza Trump.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema amesikitishwa na uamuzi wa Trump lakini akasema anapata moyo kutoka kwa viongozi wengine duniani ambao wameamua kuendelea kutetekelez amkayaba huo.

Mataifa mengine kama Uingereza, Mexico na Fiji pia yamalaani hatua hiyo.

Mkataba wa Paris unalenga kuhakikisha kuwa mataifa makubwa yenye viwanda, vinavyotoa hewa chafu kama China na Marekani kuhakikisha kuwa mkataba huu unatekelezwa na kiwango cha joto hakiongezeki na kufikia senti dregi mbili.