DRC-POLIO-AFYA

WHO: Polio yabainika DRC

Kampeni ya chanjo dhidi ya polio katika mji wa Lubumbashi mwaka 2010.
Kampeni ya chanjo dhidi ya polio katika mji wa Lubumbashi mwaka 2010. AFP PHOTO / GWENN DUBOURTHOUMIEU

Shirika la Afya duniani (WHO) limetangaza kutokea kwa milipuko miwili ya ugonjwa wa polio nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, miezi michache baada ya nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa mwengine hatari wa Ebola, ambao ulisababisha kifo cha watu kadhaa kaskazini mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema uwepo wa maambukizi ya ugonjwa wa polio umebainika upo katika maeneo ambayo hawakupata kinga ya kutosha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Inaaminiwa kuwa maambukizi ya polio yanawashambulia zaidi vijana na athari zake ni kupooza kwa kudumu kwa baadhi ya viongo vya mwili vya binadamu.

Nchi ambazo zinakabiliwa hasa na ugonjwa huu licha ya kuwepo kwa kampeni nyingi za kuutokomeza ugonjwa huu ni Nigeria, Pakistan na Afghanistan.

Shirika la Afya Duniani linabaini kwamba kuna hatari kubwa ya ugonjwa huo kusambaa katika baadhi ya maeneo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.