MADAGASCAR-AFYA

Ugonjwa wa Tauni wadhibitiwa Madagascar

Maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Madagascar wanahamasisha wakazi kuhusu ugonjwa wa Tauni katika kata ya Soavimasoandra, Antananarivo (picha ya zamani).
Maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Madagascar wanahamasisha wakazi kuhusu ugonjwa wa Tauni katika kata ya Soavimasoandra, Antananarivo (picha ya zamani). RFI/Laetitia Bezain

Serikali ya Madagascar kupitia Waziri wake wa Afya imesema kuwa imeudhibiti ugonjwa wa Tauni. Ugonjwa huo umewaua watu 133 na kuathiri watu zaidi ya 1,200 tangu mapema mwezi Agosti kulingana na ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa na Ofisi ya Taifa ya inayokabiliana na Majanga.

Matangazo ya kibiashara

Kesi chache zimeorodheshwa katika wiki mbili zilizopita.

Kwa siku tatu mfululizo, hakuna kifo kinachohusiana na ugonjwa kilichoorodheshwa katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo. Katika mji wa Tamatave, imekuwa siku 12 hakujaripotiwa kifo cjhochote kinachohusiana na ugonjwa wa Tauni. Ugonjwa huu uliathiri miji hii ya Madagascar .

Dk. Mamy Lalatiana Andriamanarivo, ambaye ni Waziri wa Afya wa Madagascar amesema "ugonjwa wa Tauni umedhibitiwa vilivyo. Idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini inaendelea kupungua. Wale ambao walikuwa wamewasiliana na wagonjwa wanahudumiwa kwa sasa. Inabakia tu wale ni vigumu kuwakagua, ni watu wanaokataa kukubali kuwa baadhi ya ndugu zao waliambukizwa na ugonjwa huu, pamoja na wale waliokua wamelazwa hospitali na baadae wakatoroka".

Moja ya vita vya serikali ya Madagascar, ni kupambana na uvumi kuhusu ugonjwa wa Tauni unaoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.