Theresa May aomba msamaha kwa wingi wa wagonjwa katika hospitali za Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May. REUTERS/Maurizio Degl'Innocenti

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ameomba msamaha kwa maelfu ya wagonjwa ambapo zoezi la upasuaji limeahirishwa katika hali ya kupunguza idadi ya wagonjwa katika hospitali za Uingereza ambazo zimejaa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Huduma ya Afya kwa umma nchini Uingereza, National Health Service (NHS), wiki hii imetoa wito wa kuahirishwa mwezi ujao kwa zoezi la upasuaji kwa wagonjwa ambao afya yao si mbaya zaidi.

Kwa mujibu wa vyanzo vyenye mamlaka, uamuzi huu unaweza kuhusisha wagonjwa 50,000.

"Ninajua ni vigumu, najua inasikitisha, najua inauma kwa wagonjwa, na ninawaomba msamaha," Theresa May ametangaza kwenye kituo cha habari cha Sky News baada ya kutembelea hospitali moja karibu na London.

Homa, hali ya hewa ya baridi na ongezeko la magonjwa ya kupumua vimesababisha kazi kuwa ngumu kwa wafanyakazi wa hospitali nchini Uingereza katika wiki za hivi karibuni.