MAREKANI-TRUMP-TABIA NCHI

Marekani kurejea kwenye mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris

"Muisaidie", sayari: ujumbe uliotumwa wakati wa maandamano kwa niaba ya marais na viongozi wa serikali waliohudhuria mkutano kuhusu tabia nchi, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.
"Muisaidie", sayari: ujumbe uliotumwa wakati wa maandamano kwa niaba ya marais na viongozi wa serikali waliohudhuria mkutano kuhusu tabia nchi, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York. REUTERS/Carlo Allegri

Rais wa Marekani Donald Trump hapo amesema nchi yake huenda ikarejea kwenye mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris licha ya kutoweka wazi nia yake hasa ya kurejea kwenye makubaliano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Rais Trump amesema binafsi hana matatizo na makubaliano yaliyofikiwa lakini tatizo lake ni makubaliano yaliyotiwa saini akisema mara zote viongozi wa dunia wamekuwa wakikubaliana mikataba mibaya.

Mwezi Juni mwaka jana rais Trump alieleza nia ya kuiondoa nchi yake kwenye makubaliano ya Paris akisema mkataba uliotiwa saini na mtangulizi wake unainyima fursa Marekani kuwa taifa lenye nguvu.

Wataalamu wanasema mchakato wa nchi hiyo kujitoa kwenye makubaliano hayo utachukua muda na una vipengele vigumu hali inayoibua maswali ikiwa rais Trump alimaanisha kile alichokisema kuhusu kujitoa katika mkataba uliotiwa saini mwaka 2015.

Akiwa na mgeni wake waziri mkuu wa Norway Erna Solberg rais Trump amejisifu kama mpenda mazingira huku akijua madhara ya kidunia yatakayotokea ikiwa nchi yake itajitoa kwenye makubaliano ya Paris kupunguza hali ya joto la dunia.