DRC-AFYA-EBOLA

Mtu mmoja afariki baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola Butembo

Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018.
Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018. AFP/John Wessels

Ugonjwa wa Ebola unaendelea kusababisha vifo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hasa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashiriki mwa nchi hiyo. Zaidi ya watu 80 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi mkuu wa idara inayokabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, Dk. Barthe Ndjoloko, ameiambia VOA Afrique kwamba mtu mmoja amefariki baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola huko Butembo, mji mkuu wa pili katika wilaya ya Beni, mashariki mwa DRC.

Hii ni kesi ya kwanza katika mji huu. Lakini ugonjwa huu wa Ebola umeua watu wasiopungua 85, ikiwa ni pamoja na 54 waliothibitishwa katika wilaya ya Beni, mashariki mwa nchi, takwimu zilizochapishwa kwenye akaunti ya Twitter ya Wizara ya Afya zinabaini.

"Mtu huyu aliyefariki alikua na mawasiliano ya karibu na mtu mmoja aliyeambukizwa virusi vya Ebola kutoka Beni ambaye, wakati mmoja, alikataa kushirikiana na idara zetu zinazotoa huduma lakini alikwenda kujificha Butembo," amesema Dr Ndjoloko.

Wizara ya Afya, kutokana na kesi hii, imemarisha timu za wataalamu ambao wanaendelea na kazi yao katika mji huu.

"Tayari tumewatambua watu ambao wamekua na mawasiliano ya karibu na wa gonjwa wa Ebola tumeanza kuwapa kinga tangu Jumatao wiki hii na tunaendelea na uchunguzi," amesema mkurugenzi idara inayokabiliana na mlipuko wa Ebola DRC.

Licha ya kesi hii na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo , mamlaka ya afya wamejipongeza kuwa watu wengi walioambukizwa virusi vya Ebola wamepona.