DRC-EBOLA-AFYA

Idadi ya vifo kutokana na Ebola yafikia 153 mashariki mwa DRC

Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC.
Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC. Florence Morice/RFI

Idadi ya watu waliopoteza maisha Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeongezeka na kufikia 153 kulingana na ripoti ya tarehe 20 Oktoba 2018 ya shirika la Afya duniani (WHO) .

Matangazo ya kibiashara

Takwimu za hivi punde zimetolewa na Shirika la afya duniani WHO.

Wiki iliyopita, WHO ilionya kuwa, kuna hatari ya maambukizi hayo kuendelea kuenea iwapo visa vya maambukizi havutapungua.

Eneo lililoathiriwa zaidi ni mji wa Beni, katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Wiki iloyopita Shirika la afya duniani WHO lililitaka Baraza la Usalama la Umoja kupitisha bajeti zaidi ili kusaidia kukabiliana na maambukizi ya uginjwa hahtaribwa Ebola, hasa Mashariki mwa DRC.

Hata hivyo, Shirika hilo linasema maambukizi hayo hayajafikia kiwango cha kutisha na kuathiri maeneo mengine duniani.

Takwimu kutokana na mlipuko uliopo sasa wa Ebola nchini DRC, unaonyesha kwamba kati ya watu 10 walioambukizwa Ebola 6 hufariki.