DRC-KIPINDUPINDU-AFYA

Watu 857 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa kipindupindu tangu mwezi Januari DRC

Kituo cha MSF kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu nchini DRC.
Kituo cha MSF kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu nchini DRC. LIONEL HEALING / AFP

"Kesi 25,170 za kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo vya watu 857" zimeripotiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na takwimu zilizochapishwa na ofisi ya Shirika la Afya Duniani nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ugonjwa wa kipindupindu katika mwaka wa 2018 umejitokeza upya katika familia zilizopata ugonjwa huo mwaka wa 2017 lakini pia kuna familia mpya ambazo zinakabiliwa na ugonjwa huo katika mikoa mbalimbali.

Watu walioathirika zaidi ni wale wanaoishi katika "maeneo jirani ya mito mikubwa, katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji ya kunywa na matatizo ya usafi, " kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Angalau mtu mmoja anaripotiwa kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu katika mikoa 21 kati ya 26 inayounda DRC. Mikoa inayoathiriwa zaidi na ugonjwa huo ni Kasaï Mashariki, Lomami (katikati), Kivu Kusini, Tanganyika, Haut-Katanga (Mashariki).

Ugonjwa wa kipindupindu uliuawa watu 1,190 nchini DRC kwa jumla ya kesi 55,000 mwaka jana.

Kwa mujibu wa wataalamu, "jumla ya kesi 15,766 [za kipindupindu] kwa wastani zinatarajiwa ndani ya kipindi cha miezi 6 ijayo nchini DRC".

WHO inabaini kwamba chanjo kwa watu wanaokabiliwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa huo ni miongoni mwa majibu katika mpango wa kukabiliana nao.

Shughuli hii italenga watu zaidi ya milioni sita "katika maeneo hatari ya afya na dozi mbili za chanjo ya OCV" zitatoplewa hadi mwaka 2020.

Mnamo mwaka 2018, mbali na ugonjwa wa kipindupindu, DRC inakabiliwa na mlipuko wa kumi wa Ebola katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Ugonjwa ambao umesababisha vifo vya watu 212 tangu ulipozuka tarehe 1 Agosti. Ugonjwa huo unaathiri mji wa Beni, ambapo huduma kwa wagonjwa imekuwa ni vigumu kutolewa kufuatia mauaji yanayotekelezwa na kundi la waasi wa Uganda wa ADF.

Ugonjwa wa Ebola uliuawa watu 33 kwa jumla ya kesi 54 katika mkoa wa Equateur, Kaskazini magharibi mwa DRC.

Uchaguzi wa urais, wa wabunge na ule wa magavana umepangwa kufanyika Desemba 23 nchini DRC, nchi kubwa zaidi kusini mwa Jangwa la Sahara.