DUNIA-WB-TABIA NCHI

Benki ya Dunia yaahidi bilioni 200 katika suala la tabia nchi

Makao makuu ya Benki ya Dunia Washington, Marekani.
Makao makuu ya Benki ya Dunia Washington, Marekani. Wikimédia

Benki ya Dunia imeahidi kiasi cha Dola bilioni mia mbili kusaidia uwekezaji kwenye suala la mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwaka 2021-25, na kuongeza kiasi hiki kwa mara mbili ya fedha zake za sasa za ufadhili wa miaka mitano.

Matangazo ya kibiashara

Nchi zilizoendelea zimeahidi kutoa dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020 ili kufadhili sera za hali ya hewa katika nchi zinazoendelea. Lakini hata kama kiwango kimeongezwa,kwa mujibu wa OECD (Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo), nchi za Kusini zinaomba ahadi zilizo wazi kutoka Kaskazini.

Bahasha ya dola bilioni 200 iliyotangaza leo Jumatatu itakuwa na dola bilioni 100 za "fedha za moja kwa moja" kutoka Benki ya Dunia.

Nusu nyingine imegawanywa kati ya theluthi moja ya fedha za moja kwa moja kutoka kwa mashirika mawili ya Kundi la Benki ya Dunia na theluthi mbili za fedha utoka sekta za kibinafsi zilizotolewa na washirka wao, afisa anayehusika na masuala ya fedha kutoka Benki ya Dunia, John Roome, ameliambia shirika la Habari la AFP, huku akiongeza kuwa kiwango hicho kitakuwa sawa na 35% ya jumla ya fedha.

Benki hiyo inasema hatua hiyo inakwenda sambamba na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa unaokutanisha wadau wapatao 200 nchini Poland.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa unakuja katika wakati muhimu ambapo ongezeko la joto duniani linatishia kupotea kwa viumbe na uoto wa asili.