Pata taarifa kuu
AFRIKA-MALARIA-AFYA

Ugonjwa wa Malaria waendelea kusababisha vifo vingi Afrika

Licha ya juhudi za bara la Afrika kutokomeza ugonjwa wa Malaria, bado ugonjwa huo unaua mamilioni ya raia.
Licha ya juhudi za bara la Afrika kutokomeza ugonjwa wa Malaria, bado ugonjwa huo unaua mamilioni ya raia. Photo: Matibabu
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Leo ni siku ya Malaria duniani , nchini Congo Brazzaville, changa moto bado ni kubwa ambapo ugonjwa huo unagharimu maisha ya watoto wengi wenye umri wa miaka mitano na watu wazima.

Matangazo ya kibiashara

Nchini DRC katika kuutokomeza ugonjwa huo Madaktari wamejipanga kuendelea kutoa chanjo kama ambavyo malengo ya shirika la afya duniani WHO lilivyo la kumaliza ungojwa huo mpaka ifikapo mwaka 2030.

Ugonjwa huo pia umeathiri eneo kubwa la Afrika magharibi, ambapo pamoja na mataifa mengine ugonjwa huo unasababisha watoto kushindwa kwenda mashuleni na watu kushindwa kufanya kazi.

Ripoti ya WHO kwa miaka miwili mfululizo 2015-2016 limebaini kwamba zaidi ya asilimia arobaini ya raia wa DRC wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Malaria na pia, kwa muujibu wa ripoti hiyo Congo na Nigeria zimekuwa nchi za kwanza duniani kuathiriwa na ugonjwa huo.

Chanjo ya kwanza ya Malaria duniani itajaribiwa kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka ujao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.