DRC-EBOLA-AFYA

Zoezi jipya la chanjo dhidi ya Ebola lazua kizaaza DRC

Wauguzi wa WHO wakitoa chanjo dhidi ya Ebola kwa daktari kutoka DRC katika mji wa Mbandaka Mei 21, 2018, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola.
Wauguzi wa WHO wakitoa chanjo dhidi ya Ebola kwa daktari kutoka DRC katika mji wa Mbandaka Mei 21, 2018, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola. Junior D. KANNAH / AFP

Siku chache baada ya kujiuzulu kwa waziri wa Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akidai ni kutokana na kuingiliwa majukumu yake, baadhi ya wanasiasa wameeleza wasiwasi wao kuhusu taarifa za kuanza kutumika kwa chanjo ya Ebola ambayo haijafanyiwa majaribio.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huu watu zaidi ya elfu 1 na 700 wakiripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya Ebola, mbunge mmoja wa mashariki mwa nchi hiyo ameibuka na kuwataka wananchi wake kutokubali kupewa chanjo hiyo ambayo haijathibitishwa.

Muhindo Nzangi Butondo akinukuliwa na kituo komoja cha habari za kimataifa, amesema hataki kuona wananchi wake wanatibiwa kama nguruwe wa Guinea, akitaka kwanza chanjo mpya iliyoanza kutolewa ithibitishwe.

Butondo ameonya dhidi ya kutengenezwa kwa mfumo mwingine wa afya nchi humo ambao hautawajengea uwezo maofisa wa afya wa ndani, matamshi anayoyatoa baada ya waziri wa afya aliyejiuzuli Dr Olly Ilunga kuda kusikitishwa na Serikali kukubali kuanza kutumika kwa chanjo mpya ambayo haikupitia mifumo sahihi ya kiafya.

Chanjo pekee iliyokubaliwa na bodi ya maadili ya DRC na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni ile ya Merck ambayo imeonesha kuwa na ufanisi kwa asilimia 95.7 kutibu Ebola, lakini sasa kuna dawa nyingine 2 zinatakiwa kuanza kutumika.